Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Jamii

Siri nzito Arusha

Print PDF

*Mamia ya vijana wapelekwa Somalia, Darfur
*Watajwa kupewa mafunzo ya kigaidi

WAKATI Jiji la Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vijana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi.

Chanzo cha habari kutoka katika duru za usalama mkoani Arusha kimesema kuwa, vijana wanaodaiwa kwenda Somalia kwenye kambi za kundi Al-Shabab na Darfur ni wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea.

Haikuweza kufahamika mara moja ni nani au kundi gani mkoani humo au sehemu nyingine nchini limehusika kuwapeleka vijana hao katika maeneo hayo.

Alipoulizwa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Liberatus Sabas, alisema ofisi yake haina taarifa hizo, na akasema kama kuna mtu mwenye taarifa kuhusiana na vijana hao aziwasilishe.

Mara ya mwisho imehaririwa Alhamisi, Julai 11, 2013 10:37

Mauaji gerezani

Print PDF

*Mfungwa apigwa hadi kufa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Gereza
UONGOZI wa Gereza la Kisongo mkoani Arusha unatuhumiwa kuwapiga na kuwatesa wafungwa na mahabusu, kiasi cha kusababisha kifo cha mfungwa mmoja na kuwapo majeruhi kadhaa.

Vyanzo vya habari kutoka gerezani hapo vimemtaja mfungwa aliyeuawa kutokana na kipigo kutoka kwa maofisa wa magereza kuwa ni Wilfred Mallya, mfungwa namba 315 ya mwaka 2003, aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha jela.

Taarifa zimesema kuwa mfungwa huyo alipata kipigo kikali ofisini kwa Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) L.W Msomba, Januari 24, na kufariki dunia kesho yake, Januari 25 mwaka huu na baadaye mwili wake ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru.

Mara ya mwisho imehaririwa Alhamisi, Machi 21, 2013 07:34

Mhariri Kibanda aanza mazoezi

Print PDF

*Lwakatare wa CHADEMA ahojiwa na polisi kwa uchochezi
AFYA ya Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda, inaendelea kuimarika. Kibanda ambaye alitekwa na kuumizwa yupo kwenye Hospitali ya Millpark nchini Afrika Kusini ambako anapatiwa matibabu zaidi.

Mhariri Kibanda aumizwa vibaya

Print PDF

TAHARUKI TASNIA YA HABARI
*Avamiwa usiku saa 6 nyumbani Mbezi Beach Dar
*Akatwa mapanga, jicho laharibika, ang’olewa meno, kucha
*Akimbizwa Afrika Kusini kwa matibabu jana mchana
*Serikali, MOAT, TEF, wabunge, wananchi walaani vikali

MHARIRI Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, usiku wa kuamkia jana amevamiwa na kundi la watu wasiojulikana, na kujeruhiwa vibaya.

Askofu Mokiwa alikubali matokeo

Print PDF

KATIBU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Canon Dk. Dickson Chilongani, amesema tuhuma dhidi yake zinazotolewa kwamba ameshirikiana na Msajili wa kanisa hilo, Profesa Palamagamba Kabudi za kuuharibu uchaguzi wa Askofu Mkuu hazina msingi, kwani walioshindwa walikubali matokeo.

Makala zaidi...

  • Makanisa njia panda
  • Mtuhumiwa mauaji ya Mwangosi yatima
  • Mamlaka ya Bandari kunanuka

Kurasa 1 kati ya 2

  • «
  •  Mwanzo 
  •  Nyuma 
  •  1 
  •  2 
  •  Mbele 
  •  Mwisho 
  • »

Waliotutembelea