Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Nilonge Nisilonge?

Kwani Obama ameondoka na usafi wake?

Print PDF

“Tumepumua kwa ujio wa Rais wa Marekani, Rais Barack Obama. Eh bwana wee, kila siku vikumbo mitaani, mara mikokoteni, mara unakoswakoswa na gari, mara baiskeli, mara kibaka anakwapua mfuko wa huyu… tabu tupu kila mahali. “Sasa wahuni wamekimbilia Chalinze na kwingineko mpaka mwanamume huyu wa shoka atoke mjini. Si unaona, sasa nakunywa kahawa kwa raha mstarehe hapa barazani kwangu. Sina wasiwasi,” alisikika mzee mmoja akitamba eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam Jumanne ya wiki iliyopita ambayo ilikuwa siku ya pili na ya mwisho ya ziara ya Rais Obama.

Kamanda Suleiman Kova ana ndimi ngapi?

Print PDF

*Vijana wake wawatapeli pia wenye nyumba za kulala wageni Vigunguti
KAMANDA Suleiman Kova ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Huyu ni mtu mkubwa bwana. Huyu lazima aishi kwa kauli zake kwani mtu mkubwa hapaswi kubadili ndimi katika kitu kile kile, au siyo?

Uwanja wa ndege wa Mwanza na vibanda vyake!

Print PDF

*Eti ‘unatunza mila’
JIJI la Mwanza, wengine wanaliita Rock City kwa sababu ya kuzungukwa na mawe, madogo kwa makubwa, ni jiji linalosifiwa kwa usafi. Katika miaka ya hivi karibuni, jiji hili (la Mwanza) limekuwa likikua kwa kasi ya ajabu huku majengo marefu kama ya NSSF na PPF yaliyojengwa hivi karibuni katikati ya jiji hili yakiliremba kwa kukoleza uasili wake wa mawe yaliyolizunguka!

Ya Dk. Mwakyembe na ‘kuchimba dawa’!

Print PDF

*Wasafiri sasa watatembea na makopo
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, naye kaamua kulonga. Wiki iliyopita, Alhamisi kama leo, aliamua kukandia kitendo cha mabasi yanayosafirisha abiria mikoani kusimama porini na kisha kutoa nafasi kwa abiria kwenda kujisaidia haja kubwa au ndogo vichakani!

Mara ya mwisho imehaririwa Alhamisi, Agosti 09, 2012 09:44

Waliotutembelea