*Wengi hawapendi watoto wao wakumbwe vurugu mitaani
*Wengine waonya msimamo wa Lema kuhusu umeya wa Jiji
*Tume ya Uchaguzi nayo yalaumiwa kwa ‘kuahirisha’ vurugu
WAKATI utulivu ukirejea jijini Arusha na viunga vyake, uchunguzi uliofanywa na RAI umegundua wapo wakazi kadhaa wa Jiji hili waliolazimika kulikimbia kuogopa vurugu wakati wa uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita.
Uchaguzi huo uliofanyika kuziba nafasi za madiwani wanne kati ya watano walioondoka kwenye nyadhifa zao kwa sababu mbalimbali, ulimalizika kwa utulivu huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitetea viti vyote vinne vilivyopigiwa kura siku hiyo.
Rai
Wakazi Arusha wakimbia nchi
Dakika 67 za ‘birthday’ ya Mandela
LEO ni siku ya kuzaliwa ya mmoja wa mababa wa utu na uhuru mwa Mwafrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Mandela anatimiza umri wa miaka 95 leo, lakini kuzorota kwa afya ya mwamba huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, kunazifunika shangwe na nderemo zote za sherehe yake hiyo.
HOFU URAIS CCM 2015 CC, NEC kudhibitiwa
*Katiba CCM yaupa Mkutano Mkuu uamuzi wa mwisho
*Dk. Bana: Katiba mpya itabadili kanuni, Katiba za vyama
MJADALA mkali unaoendelea kuhusu uwezekano wa baadhi ya majina ya wagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukatwa na vikao vya juu vya chama hicho 2015, umechukua sura mpya.
Spika Makinda anahitaji kufungwa ‘luku’?
KWANI Spika wa Bunge, Anne Makinda, anahitaji kufungwa ‘luku’? Na ni ya nini kwa Mama huyu mheshimiwa sana? Usiulize kulikoni na amefanya nini? Si hivi majuzi ameibua mjadala ambao watu wanaojiita wa mhimili wa nne, yaani waheshimiwa wa tasnia ya habari, wameona kuwa mjadala huo hauwezi kupita vivi hivi bila kuujadili!
Dola za Obama zimalize ujangili
JULAI 2 mwaka huu, Rais Barack Obama wa Marekani alihitimsha ziara yake ya siku mbili nchini na kuahidi misaada kadha wa kadha kwa Taifa letu. Ukiacha Sekta ya Umeme ambayo ndio ilikuwa kipaumbele katika ziara hiyo, kiongozi huyo mashuhuri duniani aliahidi nchi yake itaisaidia Serikali ya Tanzania katika vita ya kutokomeza ujangili dhidi ya wanyamapori.
Makala zaidi...
- Siri nzito Arusha
- Doa uhusiano China, Tanzania
- Zitto akanusha kumlinda mfanyabiashara
- Kwani Obama ameondoka na usafi wake?
Kurasa 1 kati ya 34