MPAMBANO WA MGOMBEA URAIS CCM 2015
*Vita kali yatabiriwa kati ya Wasira, Lowassa na Nchimbi
*Mpango wa kukatwa jina la Lowassa waunganisha makundi
KATIKA hali inayooshesha kupamba moto kwa harakati za kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), makundi ndani ya chama hicho yameanza kuungana.
Mbali ya kuungana kwa makundi, pia wale wote wanaotajwa kuwania kuteuliwa, macho na nyoyo zao vimeelekezwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ambaye nguvu aliyonayo ndani ya vikao vya uteuzi inatarajiwa kutumika kumpata mgombea urais.
Ingawaje viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakipinga mjadala kuhusu mgombea urais au Rais ajaye ndani ya chama hicho kikongwe nchini, lakini mjadala huo unatajwa kufunika hata ile mijadala muhimu kwa maendeleo ya nchi.