Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Rai

Siri nzito Arusha

Print PDF

*Mamia ya vijana wapelekwa Somalia, Darfur
*Watajwa kupewa mafunzo ya kigaidi

WAKATI Jiji la Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vijana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi.

Chanzo cha habari kutoka katika duru za usalama mkoani Arusha kimesema kuwa, vijana wanaodaiwa kwenda Somalia kwenye kambi za kundi Al-Shabab na Darfur ni wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea.

Haikuweza kufahamika mara moja ni nani au kundi gani mkoani humo au sehemu nyingine nchini limehusika kuwapeleka vijana hao katika maeneo hayo.

Alipoulizwa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Liberatus Sabas, alisema ofisi yake haina taarifa hizo, na akasema kama kuna mtu mwenye taarifa kuhusiana na vijana hao aziwasilishe.

Mara ya mwisho imehaririwa Alhamisi, Julai 11, 2013 10:37

Doa uhusiano China, Tanzania

Print PDF

*Yatajwa kuwa soko kuu la meno ya tembo
WAKATI Serikali ikiongeza juhudi kukabiliana na kasi ya kutisha ya mauaji ya tembo nchini, China imenyooshewa kidole kwa kudhoofisha juhudi hizo. Akizungumza katika mahojiano na RAI, mtafiti maarufu wa tembo duniani ambaye ni Mtanzania, Dk. Alfred Kikoti, alisema China inapaswa kuchukua hatua za dharura kukomesha biashara ya meno ya tembo.

Zitto akanusha kumlinda mfanyabiashara

Print PDF

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe, amesema hana uwezo kisheria kumlinda mtu yoyote.  Zitto ambaye yupo ziarani nchini Marekani, ametoa kauli hiyo kutokana na kuenea kwa taarifa ambazo zinamuhusisha na uuzwaji wa kiwanja namba 10 kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, ambacho awali kilikuwa kinamilikwa na Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).

Kwani Obama ameondoka na usafi wake?

Print PDF

“Tumepumua kwa ujio wa Rais wa Marekani, Rais Barack Obama. Eh bwana wee, kila siku vikumbo mitaani, mara mikokoteni, mara unakoswakoswa na gari, mara baiskeli, mara kibaka anakwapua mfuko wa huyu… tabu tupu kila mahali. “Sasa wahuni wamekimbilia Chalinze na kwingineko mpaka mwanamume huyu wa shoka atoke mjini. Si unaona, sasa nakunywa kahawa kwa raha mstarehe hapa barazani kwangu. Sina wasiwasi,” alisikika mzee mmoja akitamba eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam Jumanne ya wiki iliyopita ambayo ilikuwa siku ya pili na ya mwisho ya ziara ya Rais Obama.

Kisarawe Bricks Factory chauzwa kinyemela

Print PDF

*Serikali yakaa kimya
KIWANDA cha kutengeneza matofali ya kuchoma cha Kisarawe Bricks (KIBRICO) kimeuzwa katika mazingira ya kutatanisha kwa mwekezaji mpya, Minjingu Mines & Fertiliser Ltd; RAI linataarifa hizo. Kiwanda hicho chenye ubia na Universal Electrical & Hardware kilizinduliwa mwaka 1986 na Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, huku Serikali ikiwa na asilimia 30 za hisa.

Makala zaidi...

  • Wapo maanyang’au wanaotamani ukoloni?
  • Rais Obama afukua vidonda Richmond
  • Maalim Seif sasa anuna
  • Prof Safari: Nyumba za Serikali zitarudi

Kurasa 2 kati ya 34

Waliotutembelea