Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Rai

Wanasiasa wanaivuruga Ngorongoro

Print PDF

KWA kipindi kirefu kumekuwapo na taarifa au tetesi za mgogoro kati ya wenyeji (Wamasai) wanaoishi kuzunguka na ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) dhidi ya mamlaka hayo. Wiki iliyopita, mgogoro huo ulipamba moto kiasi cha wenyeji hao kutishia kuandamana na kufunga geti la kuingilia ndani ya hifadhi hiyo Juni 1, mwaka huu, hifadhi ambayo ni miongoni mwa maajabu ya dunia.

RASIMU YA KATIBA: Upungufu waonekana

Print PDF

*Muungano wawekwa rehani, kufa wakati wowote
*Suala la wakuu wa mikoa, wilaya laacha maswali
*Walipa kodi kuumizwa na gharama za uendeshaji Serikali

JUMATATU wiki hii, rasimu ya Katiba mpya ilizinduliwa jijini Dar es Salaam, na kufungua ukurasa mpya kwa mustakabali wa Tanzania. Kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba, haikuwa ndogo kutokana na matakwa ya kujaribu kupata maoni kutoka kwa wananchi, makundi mbalimbali ya jamii, viongozi wakuu na wastaafu pamoja na wasomi.

Kimsingi Tume ya Warioba imefanya kazi nzuri kwa kufuata misingi iliyowekwa na Tume ya Nyalali, ambayo mwaka 1992 ilitafuta maoni ya wananchi kuhusu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi.

Mara ya mwisho imehaririwa Alhamisi, Juni 06, 2013 06:52

Kiti cha Spika kipewe hadhi kama cha Jaji

Print PDF

KWA muda mrefu tangu kuanza kwa Bunge la kumi chini ya Spika Anne Makinda, watu wengi wakiwemo wasomi na raia wa kawaida wamekuwa na maoni kwamba, kukosekana kwa utulivu bungeni kunatokana na kiti kuegemea upande. Hali ambayo husababisha manung’uniko kutoka upande mwingine.

Mwekezaji ni mwenye fedha, mwenye ardhi au wote wawili?

Print PDF

WIKI iliyopita nilianza kwa kujadili jinsi viongozi na wanasiasa wetu pengine kwa ushauri na ushawishi mkubwa wa mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Mataifa ya Magharibi, wamekuwa wakiwaasa wananchi hususan wa vijijini kuwakaribisha kama si kuwapigia magoti watu wanaokuja na fedha kutoka nje ya nchi waliobatizwa na kuitwa wawekezaji.

Rasimu ya Katiba mpya matarajio au usaliti?

Print PDF

NIMEISOMA rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia kusikiliza uwasilishaji uliokuwa na hekima ya Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa uzinduzi. Nimeamua kujiweka katika pande mbili za uchambuzi wangu ikiwa ni maoni binafsi.

Kurasa 4 kati ya 34

Waliotutembelea