Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Rai

Wapo maanyang’au wanaotamani ukoloni?

Print PDF

MATAMSHI ya Rais wa Awamu ya Tano Zanzibar, Dk Salmin Amour Jumaa, kwamba Afrika kuna baadhi ya viongozi na watu wanaosukumwa na nadharia ya kinyang’au wakitamani na kutaka kukumbatia ukoloni imevitikisa viunga vya siasa za Zanzibar, Tanzani na Afrika Mashariki. Kwa maoni yangu natumai amewatumia ujumbe usio na chenga akiubebesha mithaki uwafike wanasiasa, wanaharakati, wanadiplomasia na viongozi walio madarakani Barani Afrika.

Rais Obama afukua vidonda Richmond

Print PDF

*Azindua mradi wa Power Africa kwenye mitambo ya Richmond iliyokataliwa
*Zitto awabwaga Sitta, Dk. Mwakyembe, Shelukindo katika kusimamia ukweli

RAIS wa Marekani, Barack Obama, amemaliza ziara yake barani Afrika kwa kuzindua mradi mkubwa wa umeme wenye lengo la kuwapatia nishati hiyo wakazi milioni 20 katika nchi saba za Afrika muda mfupi ujao.

Mradi huo utakaogharimu dola bilioni saba za Marekani ulizinduliwa eneo la mbele ya mitambo ya kufua umeme ya Symbion, Ubungo jijini Dar es Salaam, ambayo miaka michache tu iliyopita iliwagawa Watanzania katika makundi mawili na kuzua mtafaruku mkubwa kisiasa.

Mitambo hiyo ni ile iliyoingizwa nchini kati ya mwaka 2006 na 2008 kwa nyakati tofauti na makampuni ya Richmond Development na Dowans, katika mpango wa dharula wa kuliepusha Taifa kuingia gizani kwa kukosa umeme.

Maalim Seif sasa anuna

Print PDF

*Ni baada ya viongozi wa Serikali kumsusa
*Balozi Seif naye akashifiwa

ZIPO kila dalili zinazoonyesha Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), sasa inaanza kwenda mrama, baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharrif Hamad, kulalamikia kususiwa serikalini na viongozi.

Prof Safari: Nyumba za Serikali zitarudi

Print PDF

VIONGOZI na wananchi wanaoishi kwenye nyumba za Serikali zilizouzwa miaka kadhaa iliyopita wametahadharishwa kuwa, zitarejea mikononi mwa umma wakati wowote ule. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na RAI jijini Dar es Salaam wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema sula hilo kwa sasa linasubiri muda tu.

Tanganyika kuongozwa na Waziri Mkuu

Print PDF

WAKATI wananchi wa Tanzania wakijiandaa kurejea tena kwa Serikali ya Tanganyika kama ilivyoainishwa kwenye rasimu ya Katiba mpya, kiongozi wa Serikali hiyo atajulikana kama Waziri Mkuu, Rai imebaini. Wanazuoni na baadhi ya wajumbe wa Tume ya Katiba wameieleza Rai kuwa, Katiba ya Tanganyika inayotarajiwa kutungwa, ndio itakayotamka jina la kiongozi wa nchi na kwa vyovyote vile ataitwa Waziri Mkuu, ambaye chama chake au kwa kushirikiana na vyama vingine anaweza kuunda Serikali kwa kuwa na wingi wa viti bungeni.

Makala zaidi...

  • Wanasiasa wanaivuruga Ngorongoro
  • RASIMU YA KATIBA: Upungufu waonekana
  • Kiti cha Spika kipewe hadhi kama cha Jaji
  • Mwekezaji ni mwenye fedha, mwenye ardhi au wote wawili?

Kurasa 3 kati ya 34

Waliotutembelea