*Serikali yakaa kimya
KIWANDA cha kutengeneza matofali ya kuchoma cha Kisarawe Bricks (KIBRICO) kimeuzwa katika mazingira ya kutatanisha kwa mwekezaji mpya, Minjingu Mines & Fertiliser Ltd; RAI linataarifa hizo. Kiwanda hicho chenye ubia na Universal Electrical & Hardware kilizinduliwa mwaka 1986 na Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, huku Serikali ikiwa na asilimia 30 za hisa.
Biashara
Kisarawe Bricks Factory chauzwa kinyemela
Mengine yaanikwa kampuni ya Bakhresa
SIKU chache baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya Said Salum Bakhresa, kutoa malalamiko kuhusu unyanyaswaji wanaofanyiwa , tuhuma nyingine zimezidi kuibuliwa. Tuhuma hizo zinakihusu kiwanda cha kutengeneza mikate kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Wakizungumza na RAI wafanyakazi hao na wengine ambao wamedai kufukuzwa kazi kwa ajili ya kutetea maslahi yao walisema kiwanda hicho kinaendeshwa kibabe.
Fedha za uwekezaji wa Gesi Mtwara shakani
TANZANIA itakosa matrilioni ya fedha za uwekezaji kutokana na vurugu za hivi karibuni zilizotokea mkoani Mtwara, RAI imebaini. Vurugu hizo zilitokana na baadhi ya wananchi wa mkoa huo kuandamana wakipinga mpango wa Serikali wa kujenga bomba kusafirisha gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.
Wawekezaji waanza kujiondoa Tanzania
KUFUNGWA kwa migodi ya dhahabu ya Tulawaka Biharamulo, Resolute ya Nzega, na Barrick kuwa katika mipango ya kuuza zaidi ya hisa zake asilimia 70 kwa makampuni ya madini ya China yaitwayo China National Gold Group, ni ishara kwamba Tanzania itapoteza nafasi yake kama nchi ambayo kwa kipindi cha miaka zaidi ya ishirni, imeweza kuvutia mitaji mikubwa ya kuwekeza katika uchumi wa nchi.
Idara za Uhamiaji, Kazi zawabania Watanzania
*Kamal Group yawatumia uhamiaji kuwaleta 'wataalamu' wa Kihindi
*Kiwanda kilifunguliwa na OSHA, lakini hakikufanyiwa marekebisho
*Ofisa wake anyang'anya vitendea kazi vya mwandishi wa habari
NI waza kwamba kuna kisichoeleweka katika Idara za Uhamiaji na Idara ya Kazi, kuhusu mchezo unaofanywa na baadhi ya kampuni za kigeni kuleta wafanyakazi kutoka nje kwa kisingizio cha uwekezaji.