*Atia saini Muswada wa Mabadiliko ya Sheria
*Awataka wampelekee marekebisho wanayoyataka
RAIS Jakaya Kikwete, ametia saini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Taarifa ya Rais Kikwete kusaini muswada huo, ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alipokuwa akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Rweyemamu alikuwa akijibu swali aliloulizwa na BBC kuhusu kilichozungumzwa katika mkutano wa jana baina ya Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa, uliofanyika Ikulu ya Dar es Salaam. Alisema katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete amewataka viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakimtaka asisaini muswada huo, kuwasilisha mapendekezo wanayoyataka kwake.
Rai
JK awagomea wapinzani kimbinu
Zitto airarua ruzuku ya vyama vya siasa
*Sasa aitaka Serikali kusitisha hadi hesabu zitakapokaguliwa
BUNGE limeagiza kusitishwa mara moja utoaji wa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa nchini, mpaka hapo hesabu zake zitakapokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Agizo hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, baada ya kamati yake kumaliza kukutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
M23 wajipanga upya
*Wadaiwa kuandaa vijana kuingia vitani
*Jeshi la Serikali laahidi kuwaangamiza
WIKI chache baada ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa lililopo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), kulisambaratisha kundi la waasi la M23, kiongozi wa kundi hilo, Bertrand Bisiimwa, ameibuka na kutangaza mkakati mpya wa kujiimarisha ili kurejea katika uwanja wa vita.
Tangazo hilo la Bisiimwa limekuja muda mfupi baada ya Shirika la Habari la Sauti ya Amerika (VOA), kuripoti kuwa masalia ya waasi hao wanajikusanya sambamba na kuandaa vijana wapya watakaopigana sambamba nao.
Mama wa Ufoo kuzikwa leo Kilimanjaro
MWILI wa mama mzazi wa mwandishi na mtangazaji wa kituo cha runinga cha ITV, Ufoo Saro, Anastazia Saro (58), aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwishoni mwa wiki iliyopita na mtu anayedaiwa kuwa ni mzazi mwenzake Ufoo, unatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Machame, mkoani Kilimanjaro. Mama huyo aliyepigwa risasi kadhaa za tumboni na maeneo mengine ya mwili, aliagwa jana katika Kanisa la KKKT Kibwegere lililopo Kibamba, jijini Dar es Salaam na baadaye mwili wake ulisafirishwa kwenda Kilimanjaro kwa maziko.
Waziri Huvisa atishiwa kuuawa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, amelalamika kuwa anatishiwa kuuawa na watu wasiojulikana kutokana na uamuzi wake wa kutekeleza agizo la kuzibomoa nyumba zilizojengwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi. Amesema vitisho hivyo vimemlazimu kwenda kuonana na Jaji Mkuu, Mohamed Othmani Chande, ili aharakishe kesi za vigogo wanaotakiwa kubomolewa nyumba walizojenga katika maeneo ya ufukweni.
Makala zaidi...
- Wapinzani kutinga Ikulu leo
- Maiti yakatwa kichwa kaburini
- Ndege yashindwa kuruka, yaungua moto
- Mwandishi wa ITV afanyiwa upasuaji kwa saa saba
Kurasa 1 kati ya 55