Rai

  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size

Hakuna Mzanzibari aliyezuiwa kutoa maoni

Print PDF

NIMESOMA makala zilizoandikwa na baadhi ya waandishi kwenye baadhi ya magazeti wakidai kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema atapambana na Jumuiya za kidini zinazowaelimisha wananchi ili kujiandaa kutoa maoni yao juu ya mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya.


Maneno haya kwa sehemu kubwa hayana ukweli, yamejaa unafiki, fitna, uzandiki na huku yakitaka kumuweka Dk. Shein katika ramani chafu ili aonekane ni Rais asiheshimu maoni ya wananchi, mkandamizaji na si mwanademokrasia.

Rais wa Zanzibar ni mstahamilivu sana, anayependa kumsiliza kila mmoja, kila kikundi na kila chama cha siasa. Pengine chini ya uongozi wake hadi sasa ukikaribia mwaka mmoja unusu katika Serikali ya Umoja wa kitaifa, bila ya kuyumba ni kutokana na uhodari wake.

Ni Rais anayependa kufuata misingi ya utawala bora wa sheria, anayeheshimu haki za binadamu, kutambua thamnani ya utu wa kila raia anayeruhusu uhuru wa maoni na kutambua nafasi ya vyombo vya habari nchini.

Dk. Shein katika maelezo yake ametamka wazi kuwa ni lazima kila Mzanzibari atoe mawazo yake, aishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Rais ili kutoa maoni na kuelezea matakwa anayoona yatafaa kwa kuiendeleza nchi.

Tahadhari pekee aliyoiweka ni kwamba wananchi hawapaswi kujadili bila ya kuwa na hoja mkononi au kusukumwa na jazba.

Ameweka msisitizo akisema kuwa kila rai ana haki ya kuamini na kufuata imani aitakayo, kujinga na chama cha siasa akipendacho, kusema analoliamini ikiwa jambo hilo halikiuki sheria na kuvunja Katiba ya nchi.

Zanzibar katika historia yake imefanikiwa kumpata Rais asiyetokana na makundi ya hasama, asiyesikiliza ushawishi, maneno ya mitaani pia akijiweka mbali na kadhi ya maneno ya utapitapi.

Kupitia mikutano ya hadhara inayoendelea kufanywa na Chama Cha Mapinduzi hapa Zanzibar, Rais ameanza kulishwa maneno, anapakaziwa ili aonekanae ni adui mpya katika jamii, hili si jambo zuri hata kidogo.

Dk. Shein si Rais wa makundi, hatokani na makundi ya kimaslahi au ya mtazamo mpya. Ni Rais ninayeweza kusema ameingia Ikulu ya Zanzibar bila kumhonga mjumbe wa NEC ya CCM lakini pia hakumuahidi mtu yeyote kumpa cheo.

Ni Rais pekee anayeweza kumnyooshea kidole yeyote ikiwa atakosea, hana muhali na mtu, hana anayemhofia au kumuogopa. Hatokani na makundi yenye msuguano uliotishia kuhatarisha uhai wa CCM au unaoendelea kumomonyoa uhai wake hadi sasa.

Jumuiya ya Uamsho hawezi kumuondoa Rais na Serikali zake, haiwezi kuvunja Muungano uliopo kwa kuwa haina jeshi, silaha wala madaraka yeyote. CCM ni chama kikubwa, chenye viongozi wengi wenye heshima na taadhima zao.

Chama hicho kwa nijuavyo kina viongozi wengi waliopevuka, wenye uwezo, akili na ujuzi wa kujibu mambo yoyote kwa nguvu ya hoja bila kuongozwa na matusi au kashfa CCM si chama cha siasa chenye kundi la wahuni, hakina watu wenye uhodari wa kutukana kinyume na ustaarabu wake wa asili tokea enzi za siasa za vyama vya TANU na ASP.

Siku zote CCM husimama kwa kujiamini kama CCM, kikijua kinafanya nini, kinajibu hoja zipi, kwa wakati upi na zaidi kwa faida na kuangalia maslahi ya jamii kuliko kumtazama mtu na kundi lake.

Vyovyote itakavyokuwa CCM bado ni chama imara, kinachoungwa mkono na wananchi wengi wa mjini, shambani na Wazanzibari wengi wanakiheshimu na kukipenda chama hicho kutokana na historia ya ASP iliyowaletea heshima na utu wao mwaka 1964.

Hali ya mambo sasa iko kinyume kabisa kwa baadhi ya viongozo wetu hapa Zanzibar. Mimi ni mwanachama wa CCM tokea ASP, si yule mkereketwa matusi, mwanasiasa chuki, mpenda ubaguzi na kutamani utengano.

Siku zote hujihesabu kama mwanasiasa ninayejithamini na kuamini nguvu ya hoja huku nikiwapuuza wanaoripuka na kutukana wenzao hadharani kama afanyavyo Mwenyekiti wetu wa CCM wilaya ya Mjini Borafia Silima Juma na Baraka Mohemed Shamte.

Nimehudhuria mkutano wa hadhara wa chama chetu kwenye uwanja wa Komba wapya, wana CCM walikusanyika kwa wingi ili kusikiliza majibu yenye mantiki yakitoka kwa viongozi wao, waliwategemea viongozi wao waweze kujibu nukta kwa nukta dhidi ya matamshi yayotolewa kwenye mikutano ya Jumuiya ya Uamsho.

Badala yake yakaanza kuporomoshwa matusi, matamshi ya kibaguzi ya kukebehi wenzetu wa Pemba. Ndani ya CCM kila kabila limo, watu wenye rangi tofauti na imani mbalimbali za kidini.

Nimeshangaa kuwasikia viongozi wa CCM wakiwataka wapemba warudi kwao kisiwani Pemba ikiwa wanataka Serikali tatu kwa madai ya kuwafuata Uamsho. Haya hayakuwa majibu tuliyoyategemea kusikia ila ni uhuni mtupu uliofanyika siku hiyo.

Wanachama wengi wenye adabu na heshima zao waliukimbia mkutano ule kabla haujesha kwani walitegemea kusikia sera na mipango imara ya chama kumbe haukuwa mkutano wa hadhara wa aina hiyo, ila ni muhadhara uliokuwa na maneno ya matusi kama wafanyavyo mabaradhuli kwenye ngoma yao ya baikoko, sunsumia au chakacha.

Si kweli kama wapemba wote wanakifuata na kukiunga mkono chama cha CUF, ni uongo mtupu, unaposema wapemba ndiyo wanaotaka Serikali tatu hivyo warudi kwao ni kuwajengea chuki wale waliomo CCM hadi sasa.

Viongozi wetu wanatakiwa kupima, kufanya tafakuri ya kutosha kabla hawajapanda majukwaani ili kuwahutubia wananchi kwa kutoa matamshi yanayoweza kutugawa na kutupunguzia idadi ya vote.

Pemba kwa mara ya tatu sasa CCM inapata kura zisizodi 21,000, hizi si kidogo, bila ya vote hizo tusingaliweza kupata ushindi japo huo mwembembe. Kuendelea kuwakebehi wapemba kwa maneno yasiyo na maana ni kuwalazimisha wakipigie vote chama cha upinzani.

Ifahamike kuwa tunapowakebehi na kuwadhalilisha wapemba majukwaani, tukumbuke kuwa hata Rais aliyepo madarakani ni mtu kutoka Pemba, viongozi wetu wote wa juu wameona Pemba, wamejukuu huko na sasa Mpemba na Muunguja ni ndugu wa damu.

Sitaki niseme kuwa hakuna wapemba wasiokataa Muungano, wapo, wanafahamika kwa idadi yao ila CCM kama chama kikubwa hakipaswi kuwa cha kwanza kusema kuwa wapemba waondoke au wahame kurudi Pemba.

Hata Rais wa kwanza Mzee Abeid Amani Karume ukizisikiza hotuba zake kabla na baada ya Mapinduzi anakemea sana hatari ya ukabila, ubaguzi na kuamini kwa ajili ya rangi ya mtu au koo zao.

Waarabu wa Oman laiti wasingeliweza kuwabagua wenyeji, wangekubali kuoana nao na kuzaliana, kuwapatia huduma za jamii kama elimu, afya, barabara ikiwa ni pamoja na wao kukubali kuwafudisha wenyeji lugha yao, nafikiri isingewezekana kuwapindua.

Kinachoonekana waarabu hao waliowabagua sana wenyeji, waliwatenga, waliwakebehi na kuwaona si lolote si chochote kama wafanyavyo baadhi ya viongozi wa CCM leo.

Najiuliza sana hivi mambo haya maovu yakifanyika huyu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ali Vuai Ali yuko wapi, anafanya nini ili kuinusuru hali hiyo isiendelee, au bado anaongozwa na makundi ya uraisi ya mwaka 2010?

Sote tunajua kuwa kila kundi mmoja lilikuwa na mgombea wake wa urais mfukoni mwaka 2010, hata mie nilikuwa na wangu, lakini alipotangazwa aliyeshinda sikutaka kubaki na dukuduku moyoni, haya yanayofanyika sasa bila shaka ni matokeo ya upinzani wa kambi yakilenga kumfuja Dk. Shein.

Nilitegemea sana niliposikia jina la Vuai limeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, nilifikiri ataepuka siasa za makundi, pia nilitegemea angeacha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini

Maoni  

 
0 #2 KISOGO DOGO 2013-05-15 10:12
Tatizo la wazanzibari sio kuzuiwa tu kutoa maoni yao, bali kuwa na hakika maoni yao yaliyo ya wengi yanaelekea kubezwa na kudharauliwa. Hili ndilo tunda baya ambalo mda huu linaendelea kupea likipevuka kwa sura ambayo sio walioitaka wazanzibari waliowengi nadhani hapo tutaona kasheshe zao.
Viongozi wenye ubaguzi ni wale ambao kupewa kwao kwa nafasi kulitokana na siasa zao za matusi walizokulia nazo kipindi ambacho matusi hapo zamani yalikuwa dili kwenye siasa za Zanzibar, hawana elimu, hekima wala ujuzi wa mambo. Kelele zao ndio kulikowapa nafasi jambo ambalo ni dhambi kubwa waifanyayo chama tawala tokea zamani.
Nukuu
 
 
0 #1 Jecha 2012-10-05 11:15
Naam hapo umesema hata nami namshangaa sana huyu Borafia au siku ile alinusa chupa kidogo kwa kiongozi kama yeye hakuapsawa kutoa matusi bali kujibu hoja.Nakubalian a nawe mwandishi hata mimi niliondoka sikuwa haja ya kuendelea kuwepo kusikiliza matusi. hata hivyo bora alivyoondoka katika nafasi hiyo
Nukuu
 

Toa Maoni


Waliotutembelea