*Wengi hawapendi watoto wao wakumbwe vurugu mitaani
*Wengine waonya msimamo wa Lema kuhusu umeya wa Jiji
*Tume ya Uchaguzi nayo yalaumiwa kwa ‘kuahirisha’ vurugu
WAKATI utulivu ukirejea jijini Arusha na viunga vyake, uchunguzi uliofanywa na RAI umegundua wapo wakazi kadhaa wa Jiji hili waliolazimika kulikimbia kuogopa vurugu wakati wa uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita.
Uchaguzi huo uliofanyika kuziba nafasi za madiwani wanne kati ya watano walioondoka kwenye nyadhifa zao kwa sababu mbalimbali, ulimalizika kwa utulivu huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitetea viti vyote vinne vilivyopigiwa kura siku hiyo.
Habari za Kitaifa
Wakazi Arusha wakimbia nchi
Dakika 67 za ‘birthday’ ya Mandela
LEO ni siku ya kuzaliwa ya mmoja wa mababa wa utu na uhuru mwa Mwafrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Mandela anatimiza umri wa miaka 95 leo, lakini kuzorota kwa afya ya mwamba huyo wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, kunazifunika shangwe na nderemo zote za sherehe yake hiyo.
HOFU URAIS CCM 2015 CC, NEC kudhibitiwa
*Katiba CCM yaupa Mkutano Mkuu uamuzi wa mwisho
*Dk. Bana: Katiba mpya itabadili kanuni, Katiba za vyama
MJADALA mkali unaoendelea kuhusu uwezekano wa baadhi ya majina ya wagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukatwa na vikao vya juu vya chama hicho 2015, umechukua sura mpya.
Dola za Obama zimalize ujangili
JULAI 2 mwaka huu, Rais Barack Obama wa Marekani alihitimsha ziara yake ya siku mbili nchini na kuahidi misaada kadha wa kadha kwa Taifa letu. Ukiacha Sekta ya Umeme ambayo ndio ilikuwa kipaumbele katika ziara hiyo, kiongozi huyo mashuhuri duniani aliahidi nchi yake itaisaidia Serikali ya Tanzania katika vita ya kutokomeza ujangili dhidi ya wanyamapori.
Siri nzito Arusha
*Mamia ya vijana wapelekwa Somalia, Darfur
*Watajwa kupewa mafunzo ya kigaidi
WAKATI Jiji la Arusha likiwa bado na kumbukumbu ya milipuko miwili ya mabomu, imebainika kuwa zaidi ya vijana 200 wapo nchini Somalia na jimboni Darfur, Sudan kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kigaidi.
Chanzo cha habari kutoka katika duru za usalama mkoani Arusha kimesema kuwa, vijana wanaodaiwa kwenda Somalia kwenye kambi za kundi Al-Shabab na Darfur ni wenye umri kuanzia miaka 15 na kuendelea.
Haikuweza kufahamika mara moja ni nani au kundi gani mkoani humo au sehemu nyingine nchini limehusika kuwapeleka vijana hao katika maeneo hayo.
Alipoulizwa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Liberatus Sabas, alisema ofisi yake haina taarifa hizo, na akasema kama kuna mtu mwenye taarifa kuhusiana na vijana hao aziwasilishe.
Makala zaidi...
- Doa uhusiano China, Tanzania
- Zitto akanusha kumlinda mfanyabiashara
- Kisarawe Bricks Factory chauzwa kinyemela
- Wapo maanyang’au wanaotamani ukoloni?
Kurasa 1 kati ya 10
- «
- Mwanzo
- Nyuma
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- Mbele
- Mwisho
- »