*Kamal Group yawatumia uhamiaji kuwaleta 'wataalamu' wa Kihindi
*Kiwanda kilifunguliwa na OSHA, lakini hakikufanyiwa marekebisho
*Ofisa wake anyang'anya vitendea kazi vya mwandishi wa habari
NI waza kwamba kuna kisichoeleweka katika Idara za Uhamiaji na Idara ya Kazi, kuhusu mchezo unaofanywa na baadhi ya kampuni za kigeni kuleta wafanyakazi kutoka nje kwa kisingizio cha uwekezaji.
Huku maelfu ya vijana nchini wakiwa wanashinda vijiweni kwa kukosa ajira, baadhi ya makampuni ya kigeni yanaleta watu kutoka nje kwa kisingizio kwamba watu hao ni wataalamu wa kiufundi.
Pamoja na kuingia nchini na kupewa vibali vya kufanya kazi, Rai limegundua udanganyifu unaofanywa na kampuni za Kamal za jijini Dar es Salaam.
Kampuni hizo kwa ujanja wa makusudi, huzuia nafasi za kiufundi katika viwanda vyake vyote na kuleta wafanyakazi wa Kihindi kutoka India, huku Watanzania wakisota mitaani.
Lakini Rai imegundua pia kwamba kuna udhaifu wa kiutendaji katika Idara ya Uhamiaji, ambayo haifuatilii na kuthibitisha kwamba
Maoni